Serikali ya Ethiopia yasema vikosi vyake vimeukamata mji wa Idaga Hamus

 


Vikosi vya serikali ya Ethiopia vimeukamata mji wa Idaga Hamus ulioko kilomita 97 kutokea mji unaodhibitiwa na waasi wa Mekelle, katika jimbo la Tigray. 


Kikosi kazi cha serikali kimearifu hii leo kupitia twitter kwamba wanajeshi waliudhibiti mji huo wa Idaga Hamus ulioko katika barabara inayotokea Adigrat hadi Mekelle. Kimesema wanajeshi hao sasa wanasonga mbele kuelekea kuukamata mji wa Mekelle ambao ni mkubwa katika jimbo la Tigray, ambalo ndilo lengo la operesheni hiyo ya kijeshi. 


Shirika la habari la Reuters hata hivyo halikuthibitisha taarifa hii ya mwisho. Ni vigumu kuthibitisha madai kutoka pande zote kwa sababu mawasiliano ya simu na intaneti yamekuwa chini tangu kulipoanza mapigano Novemba 4.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items