Tetesi za soka kimataifa


 Manchester United bado wanamtaka winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho na wanajaribu pia kusaini mkataba wa kumleta kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 kabla ya mshindano ya michuano ya mwaka ujao ya kombe la Ulaya -European Championships. (90 min)

Paris St-Germain watafanya dau kwa ajili ya mlinzi wa Real Madrid na Uhispania Sergio Ramos. Ramos mwenye umri wa miaka 34- Januari yuko huku wakifanya mazungumzo na klabu kuanzia tarehe mosi. (AS)

Mbape

PSG pia wanajaribu kuongeza mikataba ya Mfaransa Kylian Mbappe, 21, na mshambuliaji Mbrazil Neymar, 28. (Goal)

Everton na Tottenham kwa pamoja zinataka kumsaini mshambuliaji wa timu ya Napoli Mpoland Arkadiusz Milik na kijana huyu mwanye umri wa miaka 26-anaweza kupatikana kwa pauni milioni 10 tu katika kipindi cha dirisha la uhamisho wa wachezaji mwezi wa Januari . (Sun)

Celtic wanataka kumsaini mlinda lango wa Manchester United na England Dean Henderson, 23, kwa mkataba wa mkopo mwezi Januari. (90 min)

Barcelona wanaangalia uwezekano wa kumchukua beki wa Arsenal na Ujerumani Shkodran Mustafi.

Adama

Kiungo wa safu ya mbele Wolves na Uhispania Adama Traore, 24, anaamini kuwa hajakubaliwa kuanza kucheza mechi kwashababu amekataa kurefusha mkataba wake katika Wolves. Mkataba wake wa sasa unaendelea hadi 2023. (The Athletic)

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 28-yni chaguo la pili la Barca kama hawataweza kumsaini mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger. (Express)

Beki wa zamani wa Chelsea na England John Terry, 39, ni mmoja wa watu wanaoweza kuchukua kazi mpya ya umeneja wa timu ya Derby County . (Mail)

Post a Comment

0 Comments