Na John Walter-Manyara
Kutokana na mvua kuendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo hapa nchini meneja wa mamlaka wa hali ya hewa mkoa wa Manyara Selva Mziho amesema kuwa katika mkoa huo mvua zitakuwa chini ya wastani hadi wastani hivyo haitokuwa na madhara yoyote kwa wananchi mkoani hapo.
Selva ameendelea kusema kuwa Mvua hizo zitadumu ndani ya miezi miwili kuanzia Novemba hadi Januari 2021.
Hivyo amewataka wakulima mkoani hapo kuanza kuandaa mashamba na kufuata ushauri unaotolewa na afisa ugani juu kilimo kutokana na hali ya mvua.
Pia amesema kama mvua itabadilika na kuwa kubwa katika mkoa huo haitokuwa na madhara lakini ni vyema wananchi chukua tahadhari mapema hasa kwa wale waishio mabondeni.
