VIDEO: IGP Sirro akutana na IGP wa Msumbiji

Mkuu wa wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Msumbiji Bernadino Rafael wamekubaliana kufanya operesheni za pamoja kukabiliana na kikundi cha watu wanaofanya uhalifu katika maeneo ya vijiji vya mpaka unaotenganisha nchi hizo mbili.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo wakati Wakuu hao walipokutana mkoani Mtwara na kufanya kikao kazi cha ujirani mwema baina ya nchi hizo mbili ambapo wote kwa pamoja wamesema wataendelea kuishirikisha jamii ili kuweza kupata taarifa zitakazosaidia kukomesha mtandao huo wa kihalifu.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items