Wananchi wafurika kupata huduma za upimaji afya katika Maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasioambukiza


Wananchi wamesema utaratibu  wa upimaji wa afya ufanyike Mara kwa mara kwa kuwa na huduma za pamoja kwani kutasaidia wananchi kujua afya zao.

Wamesema katika Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza  ni changamoto ya makundi mbalimbali katika afya ikilinganishwa na miaka nyuma iliyopita.

Akizungumza na Michuzi Blog mwanachi Joseph Marco amesema kuwa kwa sasa makundi ya vijana yako kwenye changamoto ya Magonjwa yasiyoambukiza kutokana na ulaji usiozingatia,Lishe pamoja na kutofanya mazoezi.

Amesema changamoto nyongine ni tatizo la macho huku akisema watu wanamatatizo ya kuona na foleni imekuwa kuwa kubwa.

Nae mwanaisha Abeid amesema kuwa serikali imeweka utaratibu mzuri wa kuadhimisha na kuweka huduma zote za upimaji wa afya.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items