RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa msamaha kwa wanafunzi (wafungwa) Arobainina Tisa (49) waliokuwa wakitumikia Vyuo vya Mafunzo vya Unguja na Pemba ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra zaSherehe za miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Dk. Mwinyi ametoa msamaha huo kw amujibu wa kifungu cha 59 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ,kinachompa mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa waliofungwa gerezani.
Kutokana na msamaha huo, Dk. Mwinyi ameamuru kuwa kifungo kilichobaki cha wanafunzi (wafungwa) hao walionufaika na msamaha katika vyuo vya Mafunzo vya Unguja na Pemba kuwa kipindi hicho chote kinafutwa na waachiwe huru kuanzia Januari 11.2021.
Kwa vile, Zanzibar itakuwai na sherehekea miaka 57 ya Mapinduz iMatukufu ya Januari 12, 1964 Dk. Mwinyi ameona kuwa kunasababu za kutosha za kutoa msamaha kwa walengwa wa lionufaika na msamaha huo kwa Unguja ambaoni 46 na Pemba 3.
Msamaha huo hutolewa kila mwaka katika kipindi cha sherehe za Mapinduzi matukufu, huwahusisha wanafunzi ambao ni wazee sana, wenye maradhi sugu au weny e makosa madogo ambao wamebakisha muda mfupi wa kutumikia chuoni, wanaooneshanidhamunzurichuoninakujutiamakosayao.
Wanafunziwa Chuo cha Mafunzo, wenyemakosakama vile kuuakwamakusudi, wiziwakutumianguvu, wiziwamaliyaUmma, makosayakudhalilishawanawakenawatoto, makosayadawazakulevyanawenyemakosamengiyazamanikwakawaidahuwahawapewimsamaha.
