Guterres atangaza nia ya kugombea muhula wa pili


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametangaza rasmi kuwa atawania muhula wa pili wa miaka mitano. Guterres, ambaye muhula wake wa kwanza unamalizika Desemba 31, amethibitisha nia yake hiyo katika barua aliyomtumia Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, inayosema angependa kuendelea kukitumikia chombo hicho cha kimataifa katika kutimiza malengo yake. 

Guterres alichaguliwa mwaka 2016 na wanachama 193 wa baraza hilo, kufuatia kinyang'anyiro kilichokuwa na ushindani mkali na kuchukua madaraka baada ya Ban Ki-moon. 

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linafanya uteuzi huo kwa kuzingatia mapendekezo ya Baraza la Usalama, na hivyo ni vyema kwa mgombea kupata uugwaji mkono wa wanachama wake 15 wa kudumu wenye nguvu ya kura ya turufu. 

Guterres mwenye umri wa miaka 71, tayari ameshapata uugwaji mkono wa mwanachama mmoja ambayo ni Uingereza.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items