Trump akutana na Pence wakati ukosoaji dhidi yake ukishamiri


Rais wa Marekani Donald Trump amekutana kwa mara ya kwanza na makamu wake Mike Pence, tangu wafuasi wake walipovamia majengo ya bunge jijini Washington wiki iliyopita. 

Hatua ya Trump kukutana na Pence imeashiria mshikamano baina ya viongozi hao wakati juhudi za kumshitaki rais Trump zikishika kasi.

 Trump ameelekea jimboni Texas hii leo, katika moja ya safari zake za mwisho akiwa rais. Baraza la wawakilishi linatarajiwa kupiga kura hii leo katika jaribio gumu la kumtaka Pence na baraza la mawaziri kutumia ibara ya 25 ya katiba ya Marekani, kuamua kuwa Trump hana uwezo wa kutimiza majukumu yake, na kumsimamisha Pence kama kaimu rais. 

Wakati huohuo shirika la upelelezi la Marekani FBI, limeonya kuhusu mipango ya kufanyika maandamano ya watu wenye silaha katika miji mikuu ya majimbo yote 50 nchini humo, kuelekea kuapishwa kwa Rais Mteule Joe Biden.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi