Jan 13, 2021

Israel yafanya mashambulizi makali Syria

 


Shirika linalofuatilia na kutetea haki za binadamu nchini Syria, limesema ndege za kivita za Israeli mapema leo zimefanya mashambulizi ya angani mashariki mwa Syria, yaliyowalenga wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran pamoja na ghala za silaha. 


Shirika hilo limesema watu 23 wameuwawa wakiwemo Wasyria saba na hao wengine walikuwa wapiganaji. Shirika la habari la taifa nchini Syria, SANA limesema mashambulizi hayo yamefanywa karibu na miji ya Deir el-Zour, Mayadeen na Boukamal kwenye mpaka wa Syria na Iraq. 


Afisa mmoja mwandamizi wa ujasusi wa Marekani ambaye anafahamu kuhusu shambulizi hilo ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa mashambulizi hayo ya angani yamefanywa kutokana na taarifa za kijasusi zilizotolewa na Marekani.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger