Marekani yafutilia mbali uangalizi wake wa uchaguzi Uganda


Marekani imefutilia mbali uangalizi wake wa uchaguzi nchini Uganda kwa sababu maombi yake mengi ya kupata kibali yalikataliwa. Marekani sasa inasema uchaguzi wa kesho hautokuwa na uwajibikaji na uwazi.


 Tangazo hili linatolewa wakati ambapo kuna wasiwasi unaoongezeka kuhusu uwazi wa uchaguzi huo utakaomshindanisha Yoweri Museveni, mmoja wa viongozi wa Afrika walioongoza kwa muda mrefu, na wagombea wengine kumi akiwemo Bobi Wine, mwimbaji mwenye umaarufu mkubwa. 


Chaguzi zilizopita za Uganda zilikumbwa na kamatakamata ya wapinzani na safari hii kampeni zimeshuhudia machafuko huku watu kadhaa wakifariki dunia na wagombea wa upinzani, wafuasi wao na maafisa wa kampeni wakikamatwa na kutishwa. 


Umoja wa Ulaya umesema mchakato wa uchaguzi nchini humo umechafuliwa na utumiaji wa nguvu kupita kiasi na ombi lake la kutuma waangalizi halikukubaliwa.

Post a Comment

0 Comments