https://monetag.com/?ref_id=TTIb Rais Dkt. Mwinyi ametembelea maonesho leo | Muungwana BLOG

Rais Dkt. Mwinyi ametembelea maonesho leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) na Mkewe Mama Marium Mwinyi wakizungumza na Nd.Maryam Issa Khamis (kulia) Mkaazi wa Fuoni Mambosasa walipokuwa wakiangalia vifaa vya asili kwa matumizi ya Nyumbani katika Banda la kikundi cha 'KAMBA NDEFU GROUP" walipotembelea maonesho ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 13/01/2012.


Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Marium Mwinyi alipokuwa akiangalia bidhaa mbali mbali zilizotengenezwa kutokana na Mwani na kikundi cha "UKWELI NI NJIA SAFI" chenye maskani yake Bweleo wakati  alipoungana  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati)  walipotembelea maonesho ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 13/01/2012.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Nd.Hassan Juma Reli alipowasili katika viwanja vya maonesho ya Biashara Maisara Jijini Zanzibar leo (katikati ) Mkuu wa Wilaya ya Mjini Nd,Rashid Simai Msaraka.[Picha na Ikulu] 13/01/2021.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akifuatana na Viongozi mbali mbali wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara leo,yanayoendelea katika viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar (kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Nd,Hassan Juma Reli.[Picha na Ikulu] 13/01/2021. 
 

Post a Comment

0 Comments