Kundi la IS laua watu 19 katikati mwa Syria

 


Wanamgambo wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS), wamewaua maafisa 19 wa serikali ya Syria pamoja na wanamgambo wanaounga mkono utawala huo, katikati ya mkoa wa Hama leo. 


Hayo ni kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu lenye makao yake Uingereza.Shirika hilo limeeleza kwamba miongoni mwa waliouawa kwenye shambulizi hilo la kundi la IS lililofanyika asubuhi ya leo, ni wapiganaji 19 wa serikali na washirika wake wakiwemo wapiganaji 11 wa kundi la wanamgambo liitwalo Baqir Brigade, linaloungwa mkono na Iran.


Shirika hilo limeeleza kuwa shambulizi hilo la kushtukiza la kundi la IS saa za asubuhi, lililenga vituo vya serikali mashariki mwa Hama, eneo ambalo limekumbwa na makabiliano katika siku za hivi karibuni kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo.


Kulingana na shirika la kutetea haki za binadamu, zaidi ya watu 387,000 wameuawa Syria tangu vita vilipoanza nchini humo mwaka 2011.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items