Mamia ya walimu na wanafunzi leo wamefanya maandamano katika chuo kikuu cha Myanmar dhidi ya mapinduzi ya kijeshi yaliosababisha kuondolewa kwa kiongozi wa nchi hiyo Aung San Suu Kyi.
Walimu waliokuwa wamevalia utepe mwekundu ambayo ni rangi ya chama cha Suu Kyi na wanafunzi waliokuwa wakipiga saluti ya vidole vitatu waliimba nyimbo za sifa kwa Suu.
Huku hayo yakijiri, Utawala wa kijeshi nchini humo umemtia nguvuni msaidizi mkuu wa kiongozi aliyepinduliwa, Aung San Suu Kyi, hivi leo, zikiwa ni siku kadhaa tangu mapinduzi ya kijeshi ambayo yamelaaniwa vikali na jumuiya ya kimataifa.
