Mattarella amualika Draghi kwa mazungumzo ya kuunda serikali mpya Italia


Rais wa Italia Sergio Mattarella, ametoa mwaliko kwa rais wa zamani wa Benki Kuu ya Ulaya, Mario Draghi, katika ikulu yake Quirinal mjini Rome, kwa mazungumzo leo mchana kuhusu kuunda serikali mpya.

Awali, Mattarella alitangaza kuwa majaribio ya kupata makundi ya vyama kufufua muungano uliofeli chini ya waziri mkuu aliyejiuzulu Giuseppe Conte yameshindwa.Draghi anajulikana sana kwa kuurudisha ukanda unaotumia sarafu ya Euro katika hali ya kawaida, kutoka kwenye hatari au ukingo wa kuporomoka mnamo mwaka 2012, alipoahidi kufanya chochote ili kuokoa sarafu ya euro.

Mattarella alisema moja kati ya vitu muhimu vitakavyofanywa na utawala unaokuja, ni kuweka mipango ya dharura ya namna ya kutumia zaidi ya euro bilioni 200, kutoka katika hazina ya Umoja wa Ulaya, kuepusha mdororo wa uchumi kutokana na janga la COVID-19.

Draghi hakutoa jibu la moja kwa moja kutokana na mwaliko huo na pia haikujulikana wazi ni vyama vipi kwenye bunge hilo ambalo limegawika pakubwa, vitaunga mkono serikali atakayoiongoza.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia