Na Faruku Ngonyani , Mtwara
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mtwara Thomas Salala amewahimiza madiwani wa Halmashuri ya Manispaa Mtwara Mikindani kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kusimamia makusanyo ya kodi katika kata zao.
Ameyazungumza hayo kwenye kikao cha baraza la madiwani la utekelezaji wa kazi katika kata zao kwa kipindi cha robo ya tatu mwaka 2020/21 ambapo baraza hilo la siku mbili yani leo tarehe 03 februari 2021 na kesho tarehe 04 february 2021.
Lakini pia salala amesema kuwa kwa sasa bado kwa Halmashauri ya manispaa Mtwara Mikindani haijfanya vizuri kwenye ukusanyaji wa kodi hvyo ni vyema madiwani hao sasa kwenda kusimamia vyanzo vya mapato vya halmashauri vilivyopo katika maeneo yao.
Aidha katibu tawala huyo amechukua fursa hiyo kuwataka madiwani hao kwenda kuwahimiza wazazi na walezi ambao watoto wao waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza na wale ambao wapo tayari umri wa kuanza darasa la saba hawajaripoti mashuleni ili waweze kuripoti.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa Mtwara Mikindani Shadida Ally Ndile amesema kuwa tayari maagizo hayo kama madiwani wamishayapokea na sasa wapo tayari kuyafanyia kazi ili Manispaa hiyo iweze kusonga mbele kimaendeleo Zaidi.