Rais anayepingwa Haiti awastaafisha majaji wa mahakama ya juu


Rais anayekabiliwa na upinzani nchini Haiti Jovenel Moise amewastaafisha majaji watatu wa ngazi za juu akiwemo jaji aliyechaguliwa na upinzani kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo. Hayo yameripotiwa na vyombo vya habari nchini humo. 

Moise amesaini agizo jana Jumatatu jioni la kuwastaafisha majaji hao watatu wa mahakama ya juu nchini humo. Miongoni mwa majaji hao ni Mecene Jean Loius mwenye umri wa miaka 72 ambaye ndie jaji mwenye umri mkubwa kabisa katika mahakama hiyo.

Kabla ya kustaafishwa kwa nguvu na rais anayepingwa, jaji Loius jana alikubali uteuzi wa kuwa rais wa mpito uliofanywa na wapinzani na mashirika ya kiraia. 

Maandamano yamekuwa yakishuhudiwa nchini Haiti ya kumpinga rais Moise ambapo jana waandishi habari wawili walipigwa risasi katika mji mkuu Port-au Prince.

Wafuasi wa rais huyo na wale wa upinzani wanavutana kuhusu muda ulipoanza muhula wa rais na unapopaswa kumalizika.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi