Rais Nyusi atoa msamaha kwa raia waliojiunga na wanamgambo wa Kiislamu


Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ametoa msamaha kwa raia wa nchi hiyo waliojiunga na wanamgambo wa kiislamu katika jimbo lenye utajiri wa mafuta lililopo kusini mwa nchi hiyo la Cabo Delgado.

Rais Nyusi aliahidi kwamba hakutakua na ulipizaji kisasi dhidi ya wale wanaosalimu amri na kurejea katika familia zao.

Alitoa ahadi Jumatano wakati nchi hiyo ilipokua ikiwakumbuka mashujaa wa taifa.

Msamaha huo pia ulitolewa kwa raia waliotangazwa katika kitengo cha shirika la wanamgambo wa ndani ya nchi ambao walijiunga na shirika la lenye ushirika na chama cha upinzani cha Renamo.

Takriban watu 570,000 wamelazimika kukimbia nyumba zao kutokana na mashambulio ya wanamgamboImage caption: Takriban watu 570,000 wamelazimika kukimbia nyumba zao kutokana na mashambulio ya wanamgambo

Mamia wamekuwa wakiuawa na wapiganaji wa jihadi katika jimbo la Cabo Delgado, ambao walianzisha uasi wao mwaka2 017. Takriban watu 570,000 wamelazimika kukimbia nyumba zao kutokana na mashambulio ya wanamgambo.

Kikundi cha kigaidi cha Islamic State kilidai kuhusika na mashambulio nchini Msumbiji.

Rais Nyusi aliwataka wanamgambo kutumia fursa ya mchakato unaoendelea kukabidhi silaha.

Pia alionya kwamba serikali inaweza kutumia hatua kali huku visa vya corona vikiongezeka na akaahidi kuhutubia taifa Alhamisi kuhusu janga hla corona

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi