Ukraine yafunga vituo vya runinga vinavyofadhiliwa na Urusi

 


Serikali ya Ukraine imechukuwa uamuzi wa kusitisha shughuli za vituo 9 vya runinga nchini kwa madai ya kufadhiliwa na Urusi.


Katika taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Rais nchini Ukraine, iliarifiwa kwamba uamuzi wa Kamati ya Usalama ya Kitaifa na Ulinzi kumwekea vikwazo Taras Kozak ambaye ni mwanachama wa Bunge la Ukraine, na vituo vyake vya runinga ulipitishwa.


Kulingana na vikwazo, vituo 9 vya runinga vya Taras Kozak havitaweza kuendelea na shughuli zake kwa kipindi cha miaka 5.


Rais wa Ukraine Vladimir Zelenskiy, alichapisha ujumbe kwenye mtandao wa kijamii na kusema kuwa nchi yake inaunga mkono uhuru wa vyombo vya habari, lakini haiwezi kukubali propaganda inayofadhiliwa na nchi yoyote yenye uchokozi dhidi ya Ukraine.


Msemaji wa Zelensky, Yulia Mendel, alibaini kuwa ufadhili wa vituo hivyo ulithibitishwa na Urusi na kwamba vituo vilitumika kama zana katika vita dhidi ya Ukraine.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items