Antony Blinken amemweleza mwenzake wa China Yang Jiechi kuwa Washington itasimama imara kulinda haki za binadamu na misingi ya kidemokrasia kwenye jimbo la Xinjiang, Tibet na mji wa Hong Kong.
Kwenye mazungumzo ya simu ambayo ni kwanza baina ya wanadiplomasia hao wawili wa madola yenye nguvu, Blinken pia ameitika China kulaani mapinduzi ya kijeshi nchini Myanmar na kusititiza kuwa Marekani itafanya kazi na washirika wake kuiwajibisha Beijing kwa kutishia uthabiti wa kanda ya Asia na Pasifiki.
Kwa upande wake Yang amemweleza Blinken kuwa Marekani inapaswa kurekebisha makosa ya miaka ya karibuni na kwamba pande hizo mbili zina wajibu wa kuheshimiana linapokuja suala la mifumo ya kisiasa na mwelekeo wa maendeleo.
Mahusiano kati ya Washington na Beijing yamepwaya hadi kiwango cha chini kabisa wakati wa utawala wa Donald Trumo na maafisa wa China wameelezea kwa tahadhari matumaini ya kuimarika tena chini ya utawala wa Joe Biden.
0 Comments