Na John Walter-Babati
Ili kuongeza ari kwa wanafunzi katika ufaulu, Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Babati wamekubali kuhamasisha chakula cha mchana kwa watoto wa shule za msingi katika kata 25 za Halmashauri hiyo.
Akizungumza katika baraza la madiwani april 29,2021 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Babati John Noya, amemwagiza amesema ili kuhakikisha suala hilo linafanikiwa amemwagiza mkurugenzi mtendaji kutoa muongozo kwa njia ya maandishi kwa madiwani na watendaji.
"Ili iwe msaada kwa Madiwani wanapokwenda kufanya uhamasishaji angalau kuwe na barua kutoka kwa mkurugenzi ambayo ni muongozo kwamba suala la chakula kwa halmashauri yetu ya Babati ni jambo la lazima" alisema Noya
Amesema wao kama Madiwani wana uwezo wa kuhamasiha kwa kukaa na kamati za shule na vikao na wazazi ila kwa sasa wanataka barua maalum ya maagizo kutoka kwa mkurugenzi.
Nao madiwani walimuunga mkono Mwenyekiti kwa kupiga makofi kuonesha kukubali azimio hilo.
