Naibu Waziri Ndejembi atangaza watumishi 90,000 Nchi nzima kupandishwa madaraja


Serikali kupitia kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Utumishi, Deo Ndejembi imeahidi kuwapandishia madaraja watumishi wa umma wapatao 90,000 Nchi nzima lengo likiwa kuonesha namna wanavyowajali huku akiwataka na wao kutimiza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa weledi.

" Siyo mnachekelea kuona sisi serikali tunawapandishia madaraja ilihali nyie utendaji wenu wa kazi, Ofisi ya Rais-Utumishi haitomvumilia mtumishi yeyote ambaye ataleta uzembe kazini haitomvumilia Afisa Utumishi yeyote atakayekua akiwaonea watumishi wa umma.

Nisisitize tubadilike, haya malalamiko yanayotolewa kwa Maafisa Utumishi kuwa hawapeleki kwa wakati changamoto za watumishi wao kwenye mamlaka husika, hawatumi majina ya watumishi wanaopaswa kupandishwa Daraja, hii changamoto tumeiona Nchi nzima nirudie tena hatutovumilia wale wote wanaojiona miungu watu.

Wapo watumishi wasio waadilifu hawa niwahakikishie sisi hatutowaacha tutaruka nao, mfano hapa Chamwino nafahamu kuna Afisa Ardhi, anaitwa Charles Laseko ambaye ameuza eneo la Wananchi wa hapa kimakosa tena bila kuzingatia sheria za kazi nikuagize Mkurugenzi wa Halmashauri kumuandikia barua kali ya onyo na nakala niipate, yoyote ambaye ataenda kinyume tutamshughulikia," Amesema Naibu Waziri Ndejembi.

Post a Comment

0 Comments