Rapa Joh Makini ang'ara usiku wa kuamkia leo kwenye tuzo za MTN HipHop Awards nchini Uganda kupitia kipengele cha Kolabo Bora ya Mwaka.
Joh ni miongoni mwa washindi kupitia ngoma aliyoshirikishwa na rapa @naviomusic pamoja na Flex D' Paper iitwayo "Abaama Beeka".
Mbali na kipengele hicho, @johmakinitz pia alikua akishindanishwa kwenye vipengele vifuatavyo; Msanii bora wa mwaka na Wimbo bora wa mwaka kupitia wimbo "Dangerous".
