Waziri Mkuu wa zamani wa Uttarakhand nchini India asema virusi vya corona ni viumbe hai vyenye haki ya kuishi

Waziri Mkuu wa zamani wa jimbo la Uttarakhand kaskazini mwa India Trivendra Singh Rawat, alisema kuwa virusi vya corona (Covid-19) ni viumbe hai ambavyo vina haki ya kuishi.

Trivendra Singh Rawat, waziri mkuu wa zamani wa jimbo la Uttarakhand, alizungumza na kituo cha kibinafsi cha Runinga na kusema,

"Kwa mtazamo wa falsafa, virusi vya Covid-19 ni viumbe hai. Vina haki ya kuishi kama sisi.”

Rawat aliongezea kusema,

"Watu wanafikiri sisi wenyewe ni viumbe wenye akili zaidi na tunajaribu kuviondoa. Virusi pia vinajibadilisha kila wakati. Watu wanahitaji kuchukuwa hatua za haraka zaidi ili kuweza kujikinga na Covid-19."

Wakati ambapo India ilikuwa ikipambana na wimbi la pili la Covid-19, Rawat alidhihakiwa kwenye mitandao ya kijamii kwa taarifa zake zisizo za kawaida kuhusu virusi vya corona.

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items