CRDB yazindua kampeni ya tupo mtaani kwako inayohamasisha wananchi kutumia huduma za kibenki


Na Ezekiel Mtonyole - Dodoma.

BENKI ya CRDB imezindua msimu wa pili wa kampeni ya 'Tupo Mtaani kwako'  ambayo inalenga kuhamasisha matumizi ya huduma za  benki pamoja na kuwaunganisha watanzania walio wengi hasa wajasiliamali kutumia huduma za kibenki ili kuchochea kasi ya maendeleo.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo,Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana,Patrobas Katambi ameitaka Benki hiyo kuishirikisha Wizara ili iweze kutoa maelekezo  katika ofisi za Mikoa na Wilaya ili  ziwakutanishe na makundi yote ya kina mama,bodaboda,wajasiriamali  ili waone  jinsi ya kunufaika.


"Katika kipindi cha pili cha awamu hii CRDB tupo mtaani kwako nitaomba sana mtushirkishe pia sisi katika Wizara kwani tutatoa maelekezo  katika ofisi za Mikoa na Wilaya ili ziende zikawakutanishe na makundi yote ya kina mama,bodaboda,wajasiriamali na watu wenye mahitaji maalum ili muone jinsi ya kunufaika,"amesema katambi.

Mhe.Katambi ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuja na kampeni hiyo kwani anaamini itaweza kutoa ajira kwa vijana wengi nchini kuweza kufika mitaani kuwashawishi watanzania kufungua akaunti.

"CRDB wanatuambia Serikali tunasukuma sera na sheria wajibu tulionao ni kuhakikisha Mabenki yote nchini yanashusha riba katika mikopo na CRDB mmefanya hivyo kuhakikisha kunakuwa na fedha za kuwasaidia wananchi ili kufanya uchumi na kujipatia kipato watoe msaada rafiki.

"Wapo vijana wamefikia katika kada na wameweza kujiajiri wapo watu wazima walikuwa vijana hawa nao wana Programu maalum gharama ni kujaza fomu tu.Wanasema Usione vyaelea ujue vimeundwa,"amesema.

Vilevile,Naibu Waziri amewataka watanzania kuwa na utaratibu wa kutunza fedha ili waweze kujikwamua kiuchumi katika siku za baadae.

"Athari ya kutokutunza fedha wakati mwingine tuna kasumba ambazo  tunazikumbatia wenyewe Mwenyezimungu ametupa fursa nyingi na mabenki mengi lakini sisi hatutaki kuzitumia unapata  100,000 leo kwa dharura unataka kuitumia yote tunza kidogo weka basi hata 50,000 halafu nyingine teketeza hatuna utaratibu wa kutunza fedha,"amesema.

Amesema kazi za Ofisi ya Waziri Mkuu  ni kusimamia K tatu ambazo ni kusaidia vijana kufungua mitazamo,na kuhakikisha wanakuwa na ndoto za maisha.

"Tumeenda katika Halmashauri tunatoa fedha kule kama umechukua mkopo nenda CDRD watakusaidia pia wanaweza kukopesha kwa kukuongezea ili ufanye biashara kubwa zaidi pia wamekuwa wakikopesha makundi mbalimbali ya wajasiriamali,"amesema

Kwa upande wake,Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati,Chabu Mishwaro,amesema kampeni ya Tupo Mtaani kwako mwaka jana ilikuwa na mafanikio kwani waliweza kutembelea mikoa 20 na kuwafikia watanzania zaidi ya 100,000.

Amesema mwaka huu wamejipanga kuwafuata wateja pale walipo na kuwapa elimu ya fedha,uhamasishaji wa matumizi ya njia mbadala za utoaji wa huduma na kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba katika malengo.

"Nitoe rai kwa wateja wetu na watanzania kushiriki kikamilifu katika kampeni hii ya tupo mtaani kwako  lengo letu ni kuona tunawafikia watanzania wengi zaidi na kuwawezesha kunufaika na fursa ambazo zinazotolewa na Benki yao ya CRDB,"amesema.

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items