Israel na Hamas zadaiwa kutenda uhalifu

 


Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema pande zote mbili Hamas na Israel zilitenda uhalifu wakati wa vita vya mwezi Mei na linataka uchunguzi ufanyike. Katika ripoti yake iliyotolewa leo shirika hilo limesema lilichunguza mashambulio matatu yaliyofanywa na Israel ambapo raia 62 wa Palestina waliuawa. 


Kulingana na uchunguzi huo, mashambulio hayo yalifanyika kwenye sehemu ambako hapakuwapo umuhimu wa kijeshi. Uchunguzi huo umetokana na mahojiano yaliyofanywa na wapalestina kwenye Ukanda wa Gaza na kutokana na uchambuzi wa data. 


Katika upande mwingine asasi ya haki za binadamu ya Human Rights Watch imesema wapiganaji wa kipalestina nao walirusha roketi kuwalenga raia wa Israel. 


Shirika la kutetea haki za binadamu limesema askari wa Israel na wapiganaji wa kipalestina walikiuka sheria za kivita na kwamba walichokitenda kinaweza kuwa uhalifu wa kivita.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items