Takribani miaka miwili baada ya zaidi ya wanasayansi 10,000 kutoka mataifa 150 kwa pamoja kutangaza dharura ya kushughulikia athari za mabadiliko ya tabia nchi, wameurejea tena wito wao na kutaka uharaka wa utatuzi wa kitisho hicho.
Kwa mujibu wa jarida la kisayansi la
BioScience, wanasayansi hao wanasema mabadiliko yanahitajika haraka sana
kwa kuulinda uhai na dunia. Azimio lililosainiwa awali na wanasayansi
11,000 kwa sasa limengezewa nguvu na saini nyingine 2,800.
Tangu
kusainiwa kwake kwa mara ya mwanzo azimio hilo la dharura la kimazingira
2019, kumetokea majanga kadhaa ya mafuriko, majanga ya moto ya misituni
na ongezeko la joto, jambo ambalo linaonesha wazi ongezeko la athari za
kimazingira duniani.
