Harvey Elliott anatarajiwa kurudi uwanjani msimu huu


Kiungo wa Liverpool, Harvey Elliott anatarajiwa kurudi uwanjani msimu huu kwa mujibu wa daktari wa klabu hiyo, baada ya kiungo huyo kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu jana, Septemba 14, 2021.

Kinda huyo wa miaka 18 alivunjika kifundo cha mguu katika kipindi cha pili cha mtanange wa Ligi Kuu kati la Leeds United na Liverpool Jumapili iliyopita, mchezo uliomalizika kwa Liverpool kuitembezea Leeds kichapo cha bao 3-0.

Elliott sasa ataanza programu ya mazoezi mepesi chini ya daktari wa timu, wakati akitarajia kurudi uwanjani baadaye msimu huu, hakuna muda halisi uliowekwa wa kiungo huyo kurejea dimbani.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items