Iran yasema itaendelea na mazungumzo ya nyuklia Vienna

 


Wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema leo kuwa nchi hiyo bila shaka itaendelea na mazungumzo ya kuufufua mkataba wa nyuklia mjini Vienna. 

Msemaji wa wizara hiyo Saeed Khatibzadeh ametoa tamko hilo ingawa hakutaja tarehe kamili ambayo kikosi kilichoteuliwa na Rais Ebrahim Raisi kitaanza tena mazungumzo hayo. 

Wiki iliyopita Raisi alisema tena kwamba Iran itakubali mazungumzo yaliyo na malengo kama njia ya kidiplomasia ya kutatua mzozo huo wa nyuklia. 

Raisi alisisitiza kwamba hakustahili kuwa na shinikizo la aina yoyote na lengo liwe utekelezaji wa mkataba huo hasa Marekani kuiondolea vikwazo Iran.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia