Na Maridhia Ngemela, Mwanza.
Vijana wameshauriwa kujitokeza kwa wingi katika shindano la Angeline Jimbo cup kwani ni njia moja wapo ya ajira na nifursa kwa kujiingizia kipato.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ilemela Bi Aziza Isimbula ameyasema hayo wakati wa zoezi la ufunguzi wa mchezo wa robo fainali Kati ya timu ya kata ya Kirumba na timu ya kata ya Nyasaka katika viwanja vya shule ya msingi Sabasaba ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya Angeline Jimbo Cup 2021 ambapo ameiasa jamii kushiriki katika michezo kwaajili ya kuimarisha afya pamoja na kujipatia kipato kwa kujiajiri katika michezo.
"Amesema michezo ni ajira na tunaona wengi wanaojituma na kushiriki vena katika sekta hii wamefanikiwa kwahiyo unapoona mashindano ya namna hii usizubae changamka guess hata hao waliofanikiwa waliamua huku Mbunge wa Ilemela Angelina Mabula ananipa njema na vijana wetu msimuangushe jitokezeni kwa wingi maana mwisho wa siku mnufaika ni wewe"amesema Aziza.
Naye Kocha wa timu ya kata ya Kirumba Jonas Julius amesema kuwa kitendo Cha timu yake kupata ushindi wa kufuzu nusu fainali dhidi ya timu ya kata ya Nyasaka kimetokana na wachezaji wa timu hiyo kutokata tamaa mara baada ya kufungwa goli moja katika kipindi cha kwanza sambamba na kuahidi ushindi wa mashindano hayo katika hatua inayofuata huku akiomba mashabiki kuzidi kuiunga mkono timu hiyo.
Kwa upande wake Kocha wa timu ya kata ya Nyasaka Jumanne Samson amefafanua kuwa wachezaji wake hawapaswi kulalamika Kwa matokeo walioyapata kwani walipata fursa nyingi za ushindi wakashindwa kuzitumia badala yake amewataka kujipanga upya kwaajili ya msimu ujao huku akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Ilemela Kwa kubuni mashindano hayo
Timu ya kata ya Kirumba imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali dhidi ya Nyasaka baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati 4 Kwa 3 kabla ya matokeo sare ya goli moja Kwa moja katika mchezo wa dakika tisini.
