Mama ashindwa kumuokoa mume wake, ateketea kwa moto



Na John Walter-Manyara.

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Gift Mihayo (39) amefariki dunia baada ya kuteketea kwa moto usiku akiwa amelala nyumbani kwake.

Polisi wamesema tukio hilo limetokea septemba 13,2021 katika mtaa wa Nyunguu mjini Babati majira ya  saa Saba usiku. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Marrison Mwakyoma amesema, Jeshi hilo linachunguza chanzo cha moto huo uliosababisha nyumba kuungua na kupelekea kifo cha mwanaume huyo.

Aidha kamanda amesema  moto huo ulipotokea marehemu alikuwa katika hali ya kulewa kitendo kilichomfanya kushindwa kujiokoa wakati mke wake akiwaokoa watoto waliokuwa ndani ya nyumba hiyo ya kupanga.

Pia Kamanda ameeleza kuwa matukio ya nyumba kuungua moto yamekua yakitokea mara kwa mara mkoani hapo kutokana na wananchi kujiunganishia umeme pasipo kuwashirikisha TANESCO.

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items