Na Maridhia Ngemela, Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Gabriel Robert alipokuwa akifungua kampeni za kilimo cha pamba leo hii amesema kuwa msimu wa pamba hupanda mwaka hadi mwaka na miongoni mwa wilaya zinazozalisha zao hilo ni Misungwi,magu,kwimba,buchosa na sengerema watakuwa mifano bora na kuwa walimu wa kusambaza elimu ambayo italeta mabadiriko kupitia kampeni hii.
"Amesema Zao la pamba ni zao ambalo linakuza uchumi wa taifa kwahiyo tunapoamua kutoa elimu hii leo tunataka kufanya mapinduzi makubwa ya kuongoza kipato cha taifa na kwa wakulima moja kwa moja ili kufikia lengo tunalotarajia kama Mkoa wetu tunataka elimu ya kutosha katika shamba darasa hadi vijijini nawaomba washiriki muwe makini katika mafunzo mtakayopatiwa ili nanyie mkaisambaze kwa wakulima wetu nawaomba sana wakuu wa Wilaya na wakurugenzi mlioko hapa naomba elimu hii mtakayoipata hapa mkaisambaze kwa wakulima na kila afisa ugani wa kijiji awe na shamba darasa la kufundishia wakulima amesema Robert"
Renatus Lunga mkaguzi wa bodi ya pamba Mwanza amesema kuwa, elimu hiyo Ina lengo la kuongeza Tija ya kilimo cha pamba kwani wakulima wengi wamekuwa wakizalisha kidogo kutokana na kutokuwa na elimu na changamoto zingine na kupitia kampeni hii wataanza kuzalisha kwa wingi kwani Tanzania inatakiwa izalishe Tani milioni 1 ifikapo mwaka 2025 kupitia kampeni hizi wakulima wataanza kuzalisha walau kilo elfu 1000 kwa hekali1.
Amesema wakulima wanatarajia kuanza kupanda Novemba 15 mwaka huu hivyo elimu hii inatakiwa kufika kabla ya kuanza msimu huu ili wapate elimu ambayo itawaongoza na kuwapatia uelewa juu ya kupanda zao la pamba na kufikia lengo la kampeni hii na kila wilaya inatakiwa kuzalisha kama ilivyopangwa Mwanza watazalisha Tani elfu70 ,simiyu Tani laki 5 ,kwimba Tani elfu 30,magu Tani elfu20, sengerema Tani 10na misungwi Tani 10 sasa elimu mtakayoipata muipeleke kwa wakulima waipate kwahiyo leo tunatengeneza walimu wa kutosha kuhakikisha kampeni hii inawafikia wakulima amesema Lunga.
Naye Balozi wa pamba Tanzania Aggrey Mwanri alipokuwa akitoa elimu kwa wakuu wa Wilaya ,wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri amesema ni vema kufikisha elimu kwa wakulima kwani wao ndio walengwa wakubwa kwa lengo la kupata Tija katika zao la pamba ambalo ni muhimu linaliingizia Taifa fedha nyingi na linakuza uchumi wa wakulima ambao wataweza kuhudumia familia zao.
Aggrey amewaomba wakuu hao kuwasisitiza wakulima kufuata kanuni wanazopewa na wataalamu ikiwemo kupata mbengu zilizo bora,utayalishaji wa shamba,mbolea za samadi na virutubisho,kupanda kwa mistari na nafasi maalum,kupanda kwa idadi halisi ya mbegu katika kila shimo,kupunguza miche,kupalilia kwa wakati,kunyunyizia dawa ili kuzuia wadudu na kuvuna pamba mapema ili kutoiharibu kwani ikinyeshewa mvua au kupigiwa vumbi inaapotezea ubora wake.
Kwa upande wa washiriki waliopata nafasi ya kuzungumza akiwemo mkuu wa Wilaya ya Magu Salim Kali amesema wilaya ya Magu unaenda kuwa mfano bora katika zao la pamba kutokana na elimu waliyoipata juu ya zao hilo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kwimba Thereza Lusangija amesema wananchi wengi ni wakulima wa pamba ambao wamezoea kupanda mbengu kwa kurusha na kutopata mazao mengi hivyo watahakikisha elimu wanaifanyia kazi ili kuleta tija waweze kupata mazao mengi ambayo yatasaidia kipato.


