Tetesi za soka kimataifa


Mshambuliaji wa England Harry Kaane huenda akatia saini mkataba mpya na Tottenham iwapo kifungu cha kumuachilia kuondoka katika kandarasi yake kitawekwa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 awali aliamini kwamba alikuwa na makubaliano ya kiungwana na mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy kuondoka Spurs msimu huu wakati Manchester City ilipojaribu kumsaini. (Eurosport)

Kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans anasema kwamba anaweka hatma yake wazi huku akiendelea kujadiliana kuhusu mkataba wake na klabu ya Leicester. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amehusishwa na uhamisho wa Liverpool, Manchester United , Barcelona na Real Madrid.. (Sky Sports)

Tottenham na Atletico Madrid wote waliwasilisha ombi la dau la yuro milioni 90 kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez ambalo lilikataliwa na klabu ya Inter Milan msimu huu , huku Arsenal pia ikakataliwa baada ya kutoa ofa ya chini.. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Mshambuliaji wa Arsenal na England Bukayo Saka amefuatiliwa na klabu tofauti , lakini The Gunners wanasema kwamba mchezaji huyo hashikiki.. (Here We Go podcast, via Sun)

Kiungo wa klabu ya Bayer Leverkusen mwenye umri wa miaka 18 Florian Wirtz amevutia hamu kutoka kwa baadhi ya klabu za ligi ya premia pamoja na Bayern Munich. (Express)

Fursa ya Chelsea ya kumsajili beki wa kati wa Sevilla mwenye umri wa miaka 22 Jules Kounde itategemea iwapo kandarasi ya beki wa Ujerumani Antonio Rudiger na mabingwa hao wa Ulaya itatatuliwa.. (Star)

Kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, amesema kwamba alitaka kusalia katika klabu ya Liverpool , lakini akaondoka katika uhamisho wa bila malipo kuelekea PSG baada ya kuhisi kwamba ahitajiki na The Reds. (L'Equipe - in French)

Arsenal haijafutilia mbali matumaini ya kumsajili kiungo wa kati wa Lyon na Ufaransa Houssem Aouar na itamlenga mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 msimu ujao , ijapokuwa The Gunners watataabika kumleta London hadi pale watakapofuzu kwa kombe la klabu bingwa Ulaya.. (Todofichajes - in Spanish)

Tottenham inatarajiwa kuwa miongoni mwa klabu zitakazomsajili kiungo wa kati wa klabu ya Calgiari Nahitan Nandez , ambaye pia alikuwa akisakwa na Inter Milan, Napoli, Roma na Fiorentina, wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi Januari. Klabu hiyo ya Serie A ipo tayari kumuuza mchezaji huyo mwaka mpya.. (Tuttomercatoweb - in Italian)

 

Post a Comment

0 Comments