Na Timothy Itembe Mara.
JAMII imetakiwa kuchukua Tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Korona huku wakizingatia maelekezo yanayotolewa na wizara ya Afya.
Akiongea Waziri wa maji Jumaa Aweso kwenye kilele cha maadhimisho ya kumi ya Mara Day.ambayo yanaadhimishwa kila tarehe 15,Septemba ya mwaka ambayo kwa mwaka huu yamefanyikia wilayani Tarime mkoani Mara alisema jamii inatakiwa kuchukua tahadhari juu ya Covid 19.
Waziri pia alitumia nafasi hiyo kuitaka jamii inayozunguka bonde la Mto Mara kuzilinda na kuzihifadhi kingo za mto huo kwa maendeleo endelevu.
Lengo la maadhimisho hayo ni kutoa msukumo mkubwa wa kuhifadhi Bonde la Mto Mara unaoanzia milima ya mau nchini Kenya na kuishia Ziwa Victoria upande wa Tanzania.
Jambo lingine la maadhimisho hayo ni pamoja na kuendelea kulitangaza na kulifuatilia tukio mhimu la kuhama kwa wanyama katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Masai Mara nchini Kenya.
Waziri huyo alisema uchafuzi wa mazingira ikiwemo vyanzo vya maji huadhiri viumbe hai kwa hali hiyo jamii iache tabia ya kuchafua vyanzo vya maji kama vile mto Mara kwa kuwa mto huo nikichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wetu Tanzania na Kenya.
Kwa upande wake Afisa uhusiano Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria,Perepetua Masaga alisema kuwa mto Mara ni chanzo cha maji shirikishi kinachojumuisha nchi mbili za Tanzania na Kenya chanzo cha mto Mara kinaanzia katika chemchem za Enapuiyapui katika misitu iliyopo katika milima ya mau nchini Kenya na kupitia katika hifadhi ya masai Mara nchini Kenya na hatimaye kuingia hifadhi ya Serengeti (SENAPA) nchini Tanzania ukubwa wa eneo la Bonde ni 13,325km2 na urefu wa mto nitaklibani 400km.
Afisa huyo aliongeza kuwa uwepo wa mto Mara huchangia rasilimali Maji kwenye Ziwa Victoria vile vile huchangia kuwepo kwa Hifadhi ya Serengeti ambayo ni tegemeo kubwa la Taifa na wananchi jirani na hifadhi kutokana na shuguli za utalii.
Naye mkuu wa wilaya Tarime,Michael Mntenjele alisema serikali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania ilitangaza kuanza kusimamia Rasilimali za Maji kwa mfumo wa kihaidrojia ya mabonde mnamo mwaka 1981 mwaka 2000 Bodi ya maji Bonde la Ziwa Victoria ilianzishwa.
“Sisi wote tunatambua umhimu wa maji kwa maisha yetu ya kila siku ya Binadamu na viumbe wengine tunasema maji ni uhai kwa kuwa binadamu na viumbe wanahitaji maji ili waishi maji ni rasilimali mhimu sana katika kukuza na kuimarisha uchumi wa Taifa katika uzalishaji mali maji yote ni mali ya Taifa na yanasimamiwa chini ya sheria ya usimamizi wa Rasilimali za maji namba 11 ya mwaka 2009 lengo la sheria hii kuratibu na kusimamia matumizi bora ya Maji na kuzuia uchafunzi wa vyanzo vya maji”alisema Mntenjele.
Mntenjele alitumia nafasi hiyo kuitaka jamii kutunza kulinda na kudhibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji kwa kuzingatia sheria iliyopo vinginevyo atakaye bainika akikaidi sheria hiyo na kufanya shuguli za kibinadamu ndani ya mita zilizokatazwa sheria itachukua mkondowake.
Katika maadhimisho hayo Meneja mkuu wakulima wa Mara Cooperative Union (WAMAKU) Samwel Gisiboye alisema wamelipa milioni 13 kama malipo ya pili kwa mkulima ambapo kila mkulima aliweza kupata shilingi mia nne kwa kila kilo ya kahawa ya maganda,tofauti na malipo tangulizi ya shilingi 12000 kwa kila kilo ya kahawa kavu ya maganda.
