Rais Joe Biden wa Marekani amepanga kumteuwa Donald Blome, ambae kwa sasa balozi wa Tunisia kuwa mwanadiplomasiwa wa juu kabisa kwa Pakistan, kwa lengo la kudhibiti hali ya mambo katika taifa jirani la Afghanistan, kufuatia kuondoka kwa majeshi ya Marekani.
Blome nia
mwanadiplomasia mwenye ujuzi katika masuala ya kigeni na ana uzoefu wa
muda mrefu katika ukanda huo, ambapo pia aliwahi kufanya kazi katika
ubalozi mjini Kabul.
Pakistan inashiriki kwa kiwango kikubwa katika
masuala ya kidiplomasia na utawala mpya wa taifa jirani yake wa Taliban.
Na mashirika ya misaada ya kimataifa yaomeonya kwamba Afghanistan
itaingia katika janga baya la kiutu pasipo kupata usaidizi.