Ecuador yatangaza hali ya dharura kukabiliana na uhalifu

Rais wa Ecuador Guillermo Lasso ametangaza hali ya dharura katika mapambano dhidi ya uhalifu katika taifa hilo la Amerika ya Kusini. Lasso amenukuliwa kupitia hotuba yake aliyoitoa kwa njia ya televishenin kuwa, kuna adui mmoja katika mitaa ya Ecuador ambaye ni biashara haramu ya madawa ya kulevya. Hali hiyo ya dharura itadumu kwanza kwa siku 60. 
 
Miongoni mwa mambo mengine, itatoa mamlaka kwa polisi na jeshi kuhakikisha usalama mitaani hususan katika majimbo yaliyoathirika. Wakati biashara haramu ya usafirishaji madawa ya kulevya ikiongezeka, pia kumekuwa na kupanda kwa uhalifu mwingine kama vile mauaji na wizi. 
 
Zaidi ya asilimia 70 ya vifo vinavyotokea hivi sasa katika jimbo la Guayas vinahusiana na biashara ya dawa za kulevya. Siku ya Jumapili, mvulana wa miaka 11 aliuawa wakati wa makabiliano ya risasi.

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items