Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, amesema uamuzi uliotolewa hivi karibuni na Mahakama ya Katiba nchini Poland unatishia misingi ya Umoja huo na lazima utachukuliwa hatua.
Katika hotuba yake leo bungeni mjini Strasbourg, von der Leyen amesema
hukumu hiyo ni kinyume na utawala wa sheria barani Ulaya: Leyen amesema
hii ni mara ya kwanza kabisa kwamba mahakama ya nchi mwanachama inasema
kuwa mikataba ya Umoja wa Ulaya haiendani na katiba ya kitaifa.
Na hii
ina athari kubwa kwa watu wa Poland, kwa sababu uamuzi huo una athari ya
moja kwa moja kwenye ulinzi wa mahakama.
Wasiwasi umezuka kwamba kwa
uamuzi huu wa Mahakama ya Katiba ya Poland, taifa hilo nalo linaelekea
kuchukuwa hatua ya kile kiitwacho Polexit, ama kujitowa kwenye umoja wa
mataifa 27 wanachama wa Muungano wa Ulaya, kama ilivyofanya Uingereza,
Brexit.