Kamati ya Bunge la Brazil iliyoundwa kuchunguza sera ya virusi vya corona ya serikali ya rais Jair Bolsonaro itawasilisha ripoti yake leo baada ya kufanya kazi kwa muda miezi sita.
Baraza la Seneti limesema
Seneta Renan Calheiros atawasilisha ripoti hiyo inayosubiriwa kwa hamu
na umma wa Brazil, taifa ambalo lilishuhudia madhara makubwa ya janga la
virusi vya corona.
Rasimu ya ripoti hiyo ambayo tayari imesambaa
miongoni mwa vyoimbo vya habari vya Brazil inapendekeza miongoni mwa
mwambo mengine, kuwajibishwa kwa watu 70 na kampuni mbili pamoja na
kushtakiwa kwa rais Bolsonaro kwa madai ya kutenda makosa 11 ya uhalifu.
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, maseneta walijadili maudhui
ya mwisho ya ripoti hiyo hadi usiku wa manane na kuamua kuondoa tuhuma
mbili kutoka orodha hiyo.
Kamati hiyo ilianza kazi yake mwezi Aprili,
kwa dhima ya kuchunguza makosa yaliyotendwa na serikali ya rais
Bolsonaro katika kushughulikia kadhia ya janga la Corona.