Ticker

6/recent/ticker-posts

 


"Kazi haitakuwa vile mlivyozoea" - Rais Samia


Rais Samia Suluhu Hassan leo amewaapisha viongozi mbalimbali akiwemo Waziri na Naibu Waziri wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo pamoja na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na kuwataka kufanya kazi kwa kujituma kwakuwa haitakuwa kama vile walivyozoea.


"Mawaziri na Manaibu Mawaziri mnakwenda kuendelea na kazi zenu, tumeapa kutelekeza matakwa ya sheria na kanuni. Wizara yenu niliidokoa na kiapo mlichoapa hakikuwa cha wizara ambayo mnaitumikia", amesema Rais Samia.


"Kwa kipindi kama wiki tatu mlikuwa mpompo tu hamjijui, lakini leo mtakuwa tayari kuingia kwenye majukumu. Hongereni na polieni kwa kazi kwa sababu haitakuwa kama vile mlivyozoea", ameongeza.


Viongozi wengine walioapishwa ni wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ambao ni Jacob Casto Mwandegele, Magdalena Kamugisha Rwebangila na Asina Abdillah Omary.

Post a Comment

0 Comments