Mkufunzi wa
Newcastle Steve Bruce ameondoka katika
klabu ya Newcastle kwa makubaliano ya pande zote mbilisiku 13 tu baada ya Saudia kuinunua klabu
hiyo kwa £305m.
Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 60 alichukua uongozi wa klabu hiyo katika mechi yake ya 1000 akiwa mkufunzi ambapo timu yake ilishindwa 3-2 na klabu ya Tottenham – ikiwa mechi yake ya pekee kama mkufunzi wa klabu hiyo chini ya wamiliki wapya.
Bruce alisema kwamba kumekuwa na pandashukana kwamba alikuwa akitumaini kwamba wamiliki hao wapya wangepeleka mbele klabu hiyo.
Graeme Jones atachuku mamlaka ya klabu hiyo kwa muda .
Klabu hiyo imeshindwa kushinda hata mechi moja tangu ligi ya Premia ilipoanza msimu huuna imekuwa ya pili kutoka mwisho baada ya kucheza mechi nane.
Bruce aliteuliwa kuiongoza klabu hiyo mwezi Julai 2019 na kumaliza katika nafasi ya 13na 12 katika misimu yake miwili.
‘’Nashukuru kila anayehusiana na klabu ya Newcastle kwa kunipatia fursa ya kuifunza klabu hiyo’ , alisema Bruce.