Poland yazidisha askari wake mara mbili mpakani na Belarus

 


Askari wapatao 6,000 wa Poland hivi sasa wanaulinda mpaka wa nchi hiyo na Belarus, katika hatua za kuimarisha usalama, wakati wimbi la wahamiaji kutokea Belarus wakiwania kuingia Umoja wa Ulaya.


 Wizara ya ulinzi ya Poland imesema kuwa usambazaji wa vikosi vipya, unaashiria upanuzi wa kijeshi katika mpaka na kuhakikisha watu hawavuuki kinyume cha sheria. Kwa mujibu wa walinzi wa mpakani, hapo jana kulikuwa na majaribio 612 ya kuvuuka mpaka kinyume cha sheria. 


Tume ya Umoja wa Ulaya na serikali mjini Warsaw zimesema kuwa wimbi la wakimbizi limechochewa na Belarus, inayoushinikiza Umoja wa Ulaya kutokana na vikwazo ulivyoanzisha dhidi ya serikali mjini Minsk. 


Bunge pia limetisha sheria ambayo watetezi wa haki za binadamu wanasema inalenga kuwarejesha nyuma wakimbizi kinyume na sheria za kimataifa.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items