Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameanza maandalizi ya kuwachanja chanjo ya polio watoto wa umri wa chini ya miaka mitano katika maeneo yote ya Afghanistan baada ya mamlaka ya Taliban kukubali kuanza upya utekelezaji wa chanjo hiyo.
Hii ni hatua mpya ambayo itafanyika kwa mara
ya kwanza tangu 2018. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita Taliban
iliyazuia mashriki hayo katika maeneo wanayoyadhibiti kwa hofu ya
kwamba huenda ikiwa mbinu ya upelelezi inayofanywa na iliyokuwa serikali
ya Afghanistan au mataifa ya Magharibi.
Kutokana na marufuku hiyo na
mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea nchini humo, takribani watoto
milioni 3.3 wamekosa fursa ya chanjo.
Hatua hiyo ya utawala wa Taliban,
ambayo inachukuliwa katika kipindi ambacho kiwango cha polio kikizidi
kuongezeka nchini humo kinaoensha ishara ya serikali hiyo mpya kuwa
tayari kushirikiana na jumuiya ya kimatiafa.