Urusi imesimamisha ushirikiano wake wa Jumuiya ya Kujihami NATO na kuamuru kufungwa ofisi ya muungano huo ya mjini Moscow katika kile kinachoelezwa kuwa ni hatua ya kulipiza kisasi baada ya NATO kuwafurusha wanadiplomasia wa Urusi.
Mapema mwezi huu, NATO iliwaondolea idhini
wanadiplomasia wanane wa Urusi katika makamo makuu ya jumuiya hiyo mjini
Brussels, kwa kusema ina amini wanafanya kazi kwa siri kama maafisi wa
kijasusi wa Urusi.
Lakini pia umoja huo umepunguza idadi ya maafisa wa
Urusi katika makao makuu yake kutoka watu 20 hadi 10.Urusi imeyatupilia
mbali madai hayo kwa kusema hayana msingi wowote.
Na Waziri wa Mambo ya
Nje wa Urusi, Sergey Lavrov jana Jumatatu akatangaza kusitisha shughuli
za Urusi katika jumuiya ya NATO na pamoja na ofisi ya mawasiliano ya
mjini Moscow.