China leo imepinga hatua ya kuruhusu meli kubwa ya kivita ya jeshi la majini la Marekani kupita kwenye eneo la mlango bahari wa kisiwa cha Taiwan na kuitaja hatua hiyo kuwa ya makusudi ikilenga kuhujumu uthabiti wa kanda hiyo.
Jeshi la wanamaji la Marekani kwenye taarifa yake limesema meli yake hiyo ya kivita ilipita kwa njia ya kawaida kwenye eneo hilo la mlango bahari hii leo kwa kuzingatia sheria ya kimataifa.
Aidha jeshi hilo limeendelea kusema kwamba hatua yake hiyo inaonesha ni kwa namna gani Marekani inaheshimu uhuru na uwazi katika eneo hilo la Indo Pasifiki.
Hata hivyo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Zhao Lijian, amesem meli za kivita za Marekani zimekuwa zikijiimarisha na kuchochea matatizo katika eneo la mlango bahari la kisiwa cha Taiwan.