Covid: Austria yawekwa chini ya kuzuizi huku maandamano yakishuhudiwa barani Ulaya

 


Shughuli za taifa zima zimesitishwa nchini Austria huku maandamano ya kupinga amri mpya za kuzuia kusambaa kwa Covid 19 yakishuhudiwa barani Ulaya.


Tangia usiku wa manane watu nchini Austria wametakiwa kutotoka nyumbani huku maduka yasiyo ya lazima yakifungwa.


Sheria hizi mpya zimechangia kushuhudiwa kwa maandamano barani Ulaya ambapo watu wamekabiliana na polisi nchini Uholanzi na Ubelgiji.


Maambukizi yameongezeka sana barani Ulaya hali ambayo imechangia kutolewa onyo na shirika la afya duniani(WHO).


Jumamosi mkurugenzi wa kanda hiyo wa WHO Dr Hans Kluge, aliaambia BBC kuwa iwapo hatua hazitachukuliwa barani Ulaya, kama vile Za chanjo, kuvaa maski na kutumia vyeti – vifo vya watu nusu milioni vinanaweza kushuhudiwa ifikapo msimu ujao.


Wiki iliyopita Austria lilikuwa taifa la kwanza barani Ulaya kliwekea sheria suala la chanjo, huku sheria hiyo ikitarajiwa kuanza kutekelezwa mwezi Februari mwakani. Wanasiasa katika taifa jirani la Ujerumani wanajadili hatua kama hizo wakati vyumba vya wagonjwa mahututi vilifurika na visa vya juu vipya vikiripotiwa.


Hatua za kutumia nguvu kupunguza maambukizi


Ni mara ya nne amri inatangazwa Austria tangu janga hili lizuke.


Mamlama zimewaamrisha watu kukaa myumbani, iwapo hawana shughuli muhimu zikiwemo kazi, mazoezi na kununua chakula.


Migahawa, baa, vinyozi, sinema na maduka yasiyo ya lazima yamefungwa. Hatua hizi zitaendelea hadi tareje 12 mwezi Disemba licha yaa maafisa kusema zitaangaliwa tena baada ya siku 10.


Akiongea na kituo cha TV cha ORF waziri wa fedha Wolfgang Mueckstein alisema serikali sasa imeamua kuchukua hatua.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items