HRW yasema Belarus na Poland zinakiuka haki za binadamu


Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema leo kuwa walinzi wa mipaka wa Belarus wanaweza kuwa na hatia ya kuwatesa wahamiaji kwenye mpaka wa nchi hiyo na Poland na kuongeza kuwa mataifa yote mawili yametenda ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.


Katika ripoti yake, shirika hilo limesema mataifa hayo mawili yana jukumu la kuzuia vifo zaidi kwa kuhakikisha ufikiaji wa mara kwa mara wa msaada wa kibinadamu kwa watu waliokwama katika eneo hilo la mpaka. 


Watafiti wa shirika hilo la HRW wamesema wamefanya mahojiano ya kina na watu 19, ambao baadhi yao walisukumwa na maafisa wa usalama wa Poland na wakati mwingine kwa kutumia mabavu. 


Watafiti hao wamesema kuwa hatua hiyo inakiuka haki ya kutafuta hifadhi chini ya sheria za Umoja wa Ulaya na kuuhimiza Umoja huo kuanza kuonesha mshikamano na waathiriwa kwenye mpaka wa pande zote mbili ambao wanateseka.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items