Waziri wa mambo ya nje wa Yemen aliyekimbilia uhamishoni Ahmad Awad Bin Mubarak ameonya leo kwamba,hatua ya waasi kuudhibiti mji muhimu wenye utajiri wa nishati wa Marib, itakuwa ya kusababisha janga kubwa la kuporomosha bwawa lake la kale na kuuharibu ufalme mzima.
Mapambano ya kuuwania mji wa Marib huenda yataamua mwelekeo wowote wa suluhisho la kisiasa katika vita hivyo vya pili vya wenyewe kwa wenyewe tangu miaka ya 1990 nchini Yemen.
Ikiwa kundi la waasi wa Kihouthi litafanikiwa kuudhibiti mji huo basi wanaweza kuwa na usemi katika mazungumzo na hata kuendelea kuyashikilia maeneo mengine ya Kusini mwa nchi hiyo.