Wahamiaji 75 wazama katika bahari ya Mediterenia


Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM limesema kuwa wahamiaji 75 walizama katika bahari ya Mediterenia kaskazini mwa Libya mapema wiki hii walipokuwa wakijaribu kufika Italia kwa kutumia boti. 


Shirika hilo limeripoti mkasa huo wa hivi punde zaidi kupitia ujumbe katika mtandao wa twitter hapo jana kufuatia maelezo yaliyotolewa na manusura 15 waliookolewa na wavuvi na kufikishwa katika bandari ya Zuwara kaskazini magharibi mwa Libya. 


Hata hivyo halikutoa mara moja habari zaidi kuhusu tukio hilo.Pia hapo jana Jumamosi, walinzi wa pwani ya Italia waliwaokoa zaidi ya wahamiaji 420 wanaowajumuisha watoto kadhaa wa umri mdogo kutoka kwenye maboti yaliokuwa na matatizo katika bahari hiyo ya Mediterenia. 


Taarifa ya walinzi hao wa Pwani inasema kuwa watu 70 walisafirishwa na moja ya maboti yake hadi katika eneo salama katika kisiwa kidogo cha Lampedusa nchini Italia, Kusini mwa Sicily.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia