Nov 24, 2021

Macron ahakikishia kuiunga mkono Poland katika mvutano na Belarus

  Muungwana Blog       Nov 24, 2021


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron leo amemwambia waziri mkuu wa Poland Mateuz Morawieski kwamba Ufaransa na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya yanaliiunga mkono taifa hilo katika mvutano wake na Belarus lakini hiyo haimaanisha kuwa Umoja huo utapuuza wasiwasi kuhusu utawala wa sheria.


Macron na Morawiecki walifanya mazungumzo mjini Paris wakati ambapo Umoja huo unakabiliwa na kile ambacho Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen amekiita juhudi za Belarus za kuwatumia wahamiaji kuuyumbisha Umoja huo. Katika taarifa iliyotolewa, Macron amethibitisha mshikamano wake na Poland wakati inapokabiliwa na juhudi za kuiyumbisha katika mpaka wake wa Mashariki. 


Taarifa hiyo imeongeza kuwa viongozi hao wawili pia walizungumza kuhusu suala la utawala wa sheria nchini Poland.Macron alisisitiza kuhusu wasiwasi wake katika suala hilo na kutoa wito kwa serikali ya Poland kutafuta suluhu itakayolinda maadili ya msingi ya Umoja wa Ulaya.

logoblog

Thanks for reading Macron ahakikishia kuiunga mkono Poland katika mvutano na Belarus

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment