Urusi kuongeza shughuli za kijeshi kujibu hatua kama hiyo ya NATO


Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu amesema leo kuwa nchi yake inahitaji kudumisha utayari wake wa kutumia silaha za nyuklia pamoja na vikosi vyake vya kijeshi kutokana na kuongezeka kwa shughuli za Jumuiya ya Kujihami, NATO karibu na mipaka yake. 


Katika matamshi kupitia televisheni, Shiogu amesema kuwa hali ngumu ya hali ngumu ya kijeshi na kisiasa ulimwenguni na kuongezeka kwa shughuli za NATO karibu na mipaka ya Urusi zinaonyesha hitaji la uimarishaji zaidi ubora wa vikosi vyetu vya jeshi.


Nchi za Magharibi mwezi huu zimeibua wasiwasi kuhusu shughuli za kijeshi za Urusi zilizoripotiwa karibu na mpaka wa Ukraine, huku Marekani ikisema ina "wasiwasi wa kweli" juu ya ongezeko jipya la vikosi vya kijeshi karibu na mpaka huo. 


Siku ya Jumanne, Shoigu aliishtumu Marekani kwa kutuma washambuliaji wake kufanya jaribio la shmabulio la nyuklia dhidi ya Urusi kutoka mashariki na magharibi wakati wa mazoezi yake ya kijeshi ya "Global Thunder"


Post a Comment

0 Comments