Mwakilishi wa Marekani pembe ya Afrika adai vita inazorotesha suluhu ya Ethiopia

 


Mwakilishi maalumu wa Marekani kwa pembe ya Afrika, Jumanne amesema maendeleo kuelekea kupatikana muafaka wa kusimamisha mapigano kwa kuzishirikisha pande zote za mgogoro wa Ethiopia, yanapitia tishio la kutofanikiwa kwa sababu ya oparesheni za kijeshi zinazoleta mashaka.


Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba, mwakilishi wa Marekani kwa pembe ya Afrika, Jeffrey Feltman, aliwaeleza wanahabari kwa ufupi mjini Washington baada ya kurejea kutoka Ethiopia.


Mwakilishi huyo alirejea Jumatatu, ambapo alikutana na waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, na walijadili uwezekano wa suluhisho la kidiplomasia kumaliza mgogoro uliochukuwa mwaka mzima ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu na mamilioni wengine kukimbia makazi yao katika taifa hilo la pili Afrika kwa idadi kubwa ya watu.


Amesema kwamba pande zote yaani serekali ya waziri mkuu Ahmed, na TPLF wanaona kupata ushindi wa kijeshi.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items